Muna Love Arudi Tena Vitani Na Baba Patrick

Rose Alphonce maarufu kama ‘Muna Love’ amerudi tena kwenye headlines ikiwa ameingia tena kwenye mvutano na aliyekuwa mume Wake Peter Komu ‘Baba Patrick’ huku Safari hii wakipelekana

download latest music    

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa Muna Love alikwenda mahakamani ili kudai talaka yake na kugawana vitu ambavyo walichuma pamoja walipokuwa wote.

Unajua ninamshangaa sana Muna, amekwenda mahakamani, anasema ile nyumba ni ya kwake, lakini wauzaji wa kile kiwanja wapo na kama haitoshi hadi mafundi waliojenga wapo kwa hiyo tuiachie mahakama ifanye kazi yake. Talaka sawa, kama yeye ameamua, siyo mbaya kwa kuwa hawapo pamoja kwa kipindi kirefu. Kwa hiyo kama anadai talaka ni sawa tu, kwa kuwa tunasikia anahitaji kuwa huru na pengine anataka kuolewa na mwanaume mwingine”.

Baada ya tetesi hizo Gazeti la Ijumaa Lilimsaka Peter ambaye alifunguka haya kuhusu tetesi hizo:

Ni kweli nilikwenda mahakamani Magomeni (Dar) na Muna. Anataka mgawano wa mali na talaka. Ninachojua talaka zina process (taratibu) zake, lakini kesi ni tarehe 20 ya mwezi ujao (Februari) hivyo Muna anatakiwa afike na mashahidi“.

Muna na Peter waliingia kwenye mgogoro tangu walipofiwa na mtoto wao, Patrick ambapo kuliibuka mkanganyiko na sintofahamu ya kujua baba halisi wa mtoto kufuatia uwepo wa baba mwingine, Casto Dickson.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.