“Muna ni Mwanamke Shupavu Sana”- Joyce Kiria

Mtangazaji wa kipindi cha ‘Wanawake Live’ na mpiganaji wa haki za wanawake Joyce Kiria amemkingia kifua Muna Love na kumtaja kama mwanamke shupavu.

Siku chache zilizopita Muna amekuwa akikosolewa sana baada ya kuonekana amerudi Kwenye maisha yake kama kawaida baada ya Kifo Cha mwanaye Ikiwa zimepita wiki chache tu.

download latest music    

Mashabiki wamemjia juu Muna kutokana na mavazi yake ambayo amekuwa akivaa na hata kuposti picha Kwenye mitandao ya kijamii na kuendelea na maisha yake kama kawaida.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Joyce Kiria amedai Muna yuko sahihi kwa hivi sasa anavyotoka na kuonekana kwenye mitandao kabla ya kumaliza 40 ya mtoto wake aliyefariki kwa sababu hana sababu ya kuendelea kulia na kujifungia ndani kama watu wanavyomtaka.

Mimi binafsi nampongeza sana kwa kile anachokifanya sasa hivi, inaonekana jinsi gani alivyo shupavu maana bila hivyo basi angekuwa anaishi kwa maumivu makali tena ya kumsababishia athari ndani ya moyo”.

Mashabiki walimjia juu Muna baada ya kuamua kuongea na waandishi wa habari siku chache baada ya Kifo Cha mwanaye na sasa ameonekana nchini Kenya na kuendelea na maisha yake kama kawaida wakati mtoto wake hjafikisha siku 40 tangu afariki.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.