“Muziki umekuwa mgumu” Msanii mkongwe wa hip hop – Jay Moe akiri

Jay Moe amekiri kuwa wasanii wakongwe kama yeye wameondolewa kwenye ulingo wa muziki kwasababu ya mambo ya kisasa.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL ya Clouds FM, Jay Moe alieleza kuwa muziki wa sasa umekuwa na mambo mengi kama mitandao ya kijamii, photo shoot na kadhalika ambazo zimechangia kuwaondoa baadhi ya wasanii wakongwe kwenye muziki.

download latest music    
Jay Moe

“Muziki umekuwa mgumu kuliko zamani, ugumu wake ni kwamba zamani ulikuwa hauhitaji kufanya photo shoot, hauhiaji kuji-brand kwenye mitandao ya kijamii kudeal na video ukitoa tu ngoma kama Jua au Mvua, sijui Kama Unataka Demu tuliprint CD tukasambaza kwenye redio tofauti na tukahit na tukaweza kuisha. Lakini ukizunguzia muziki wa sasa hivi unaona wasanii wakali lakini wanashindwa kui ngia ndani yake sababu ya mazingira ya game ilivyo sasa hivi. Game inahitaji vitu vingi, hiyo game huwezi kuifanya mpaka uwe na pesa, mpaka kuwa sign na label kubwa ambayo inaweza kukugharamia,” Jay Moe alisema.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere