Mwana FA aeleza sababu hatafuti collabo na wasanii kutoka nje

Mwana FA ambaye ni mmoja wa wasanii ambao wanatamba sana Afrika Mashariki amedai kuwa yeye hana haja ya kufanya mziki na wasanii kutoka nje kwa sababu market yake iko bongo.

Akizungumza kwenye interview Mwana FA alisema kuwa muziki wake huwalenga Watanzania wife na hii ni kwa sababu anatakuwa burudisha. Aliendelea kwa kusema pia anaimba kwa lugha ambaye yeye mwenyewe anajua wataelewa maudhui.

download latest music    

“Aina yangu ya muziki ni kuuza maneno na lugha yangu ni kuwafikia watu wote  wale waliopo ofisini na tai zao hadi mama Tatu aliyeko Tandika na sinia lake la vitumbua, sina mahali ambapo ninaacha lakini ni hapa hapa nyumbani kwa sababu nachokiimba kina-relate na maisha yetu ya kila siku kwa upande wangu naona soko langu halipo nje ya nchi.”

Aliendelea kwa kusema,

“Wale ambao wameshafanya kazi na watu wa nje hawajakosea kwani naamini watakuwa wamejiongezea mashabiki wa nchi zingine, Good Luck to them  lakini pia wanaendelea kujitengenezea ‘Cv’ nzuri…. Lakini kwa upande wangu sijawahi kufikiria au kuweka nguvu yoyote ya kuweza kuwapata wasanii wa kimataifa, kwani hapa ndani wasanii wapo wengi na sidhani kana nitaweza kuwamaliza”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua