Mwanafunzi aliyeshtakiwa kwa kumkashifu Shilole afikishwa mahakamani

Mwanafunzi wa Chuo cha Bandari alifikishwa mahakani jana Jumatano kujibu shtaka ya kumkashifu Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole.

Thomas Lucas mwenye umri wa miaka ishirini anakabiliwa na shtaka la kumkashifu Shilole kupitia kwenye mtandao wa Instagram.

download latest music    

Upande wa mashtaka unadai kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo wakati akijiua ni kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao namba 14 ya 2016.

Shilole hata hivyo hakuweza kufika kotini kutoa ushahidi katika kesi inayomkabidhi Thomas Lucas; ilisemekana mrembo huyo hakuweza fika kotini kwasababu alikuwa anaumwa.

Kesi hiyo ya matumizi mabaya ya mtandao ilihahirishwa hadi Mei 17,2017 ambapo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere