Mwanaume wa Kuishi na Mimi Anahitaji Kuwa na Akili Hata Kama sio Mvumilivu : Amber Lulu

Mwanadada kutoka katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Amber Lulu  siku ya august 02 alikuwa akitambulisha nyimbo yake mpya katika ofisi za Clouds Media, amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye yupo single lakini anataka mwanaume mwenye akili.

Ambaer lulu ambae hapo awali aliwahi kutangaza na kusema kuwa yuko single baada ya kuachana na mwanamuziki Prezzo , anasema kuwa hataki mwanaume mvumilivu yeye anataka mwanaume mwenye akili ili aweze kuishi nae kwa sababu hata yeye ana akili nyingi sana.

download latest music    

Niko single kwa sasa na nafasi iko wazi kabisa, lakini mwanaume ambae nina mtaka inabidi awe na akili sana za kuishi na mimi, maana kuishi na mtu na mimi inahitaji akili sana hata kama hatokuwa na uvumilivu.;-Alisema Amber lulu.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.