“Mwanaume Wangu Lazima Awe na Pesa”-Miss Tanzania

Mlimbwende ambaye kushikilia taji la Miss Tanzania mwaka 2016 Diana Edward maarufu kama Diana Flave ameibuka na kudai kuwa mwanaume ambaye atakuwa na yeye Lazima awe na pesa.

Diana amefunguka na kudai kuwa mwanaume kuwa na pesa ndio kigezo kikubwa anachokiangalia kwenye mapenzi kwani anaamini kuwa mwanaume akiwa na pesa ataweza kumuhudumia vizuri.

download latest music    

Diana alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, ambapo amedai kutokana na gharama za kimaisha Miss Tanzania Lazima awe na mwanaume anayejiweza.

Pesa anazo? Ni muhimu unafikiri tunaishije mtaani Kama hana hela za kutosha, ingawa ndio mapenzi muhimu lakini na miamala lazima iwepo, Tazama Miss Tanzania wote Kama wanatoka na mtu ambaye hana pesa”.

Lakini pia Diana alikana kumuonea wivu Miss Tanzania wa sasa na kutomuonyesha sapoti kupitia mitandao ya kijamii ambapo alidai kuwa hivi sasa yupo kwenye maombi kwa ajili ya Queen Elizabeth na sio lazima amposti mtandaoni ndio watu wajue kuwa anamsapoti.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.