Mwarabu Fighter Akiri Kutelekezwa na WCB

Aliyewahi kuwa body guard wa msanii Diamond platinumz na wasanii wake kutoka WCB amefunguka na kusema kuwa tangubalipopata ajali na kuumia vibaya hakuna msanii yoyote  wa WCB aliytaka kumjulia hali wala kumpa pole lakini pengine wana jipanga kwanza.

Hata hivyo Mwarabu Fighter anasema kuwa hata pesa za matibabu na vitu vyote amekuwa akigharamia yeye mwenyewe huko akikiri kuwa ameachishwa kazi sasa ni miezi minne.Hata hivyo alioulizwa kuhusu kutelekezwa, Mwarabu Fighter alijibu kuwa neno la kutelekezwa ni kubwa sasa.

download latest music    

labda linaweza kuwa neno kali sana kusema nimetelekezwa, lakini ukweli ni kwamba sijapata huduma zozote kutoka kwa WCB,pengine wanajipanga kunisaidia sijui lakini kwa sasa ninahangaika na afya yangu mimi mwenyewe, ninashukuru ninaendelea vizuri na nina imani nitapona

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.