Mx Carter:Baraka The Prince Anahitaji Msaada,Ana Stress.

Moja ya mameneja wakubwa  nchini Mx Carter ambae kwa sasa amekuwa akimliki Shetta na Aslay , amefunguka na kuongelea tuhuma ambazo Baraka The Prince amekuwa akiwatupia wasanii wenzie kuhusu kuchezewa kwa acount yake ya you tube na kushusha idadi ya mashabiki kama alivyokuwa akilalamika mwenyewe.

Mx Carter ambae ni mmoja wa wakala ya youtube Tanzania kupitia kampuni yake ya Ngoma amesema kuwa Baraka alimfuata mwenyewe na kumwambia kuwa anataka kufuta account yake ya you tube kwa sababu hawaamini sana wasanii wenzie aliokuwa akifanya nao kazi huko na kuomba atengenezewe account mpya.Meneja huyo amesema kuwa anahisi kabisa Baraka kwa sasa atakuwa na stress hivyo  anahitaji mtu wa kuongea nae kwa msaada zaidi kwa sababu mambo anayofanya yanashangaza watu.

download latest music    

Baraka haeleweki , alinifuata akaniomba nifute hiyo account, lakini cha kushangaza anafanya interview  kila media anaongea tofauti,hata ukiangalia comments za watu wengi baada ya interview wamekuwa wakishangazwa na wanashindwa kumuelewa kitu gani kinachokuwa kinamchanganya.Ananiomba msamaha  ya kwamba amenikosea kwani alikuwa hajui kitu anakifanya, nafikiri  ana stress tunaweza kukaa chini tukamshauri ili kumsaidia.– Alifunguka Mx Carter

Akiongea na eNews ya EATV,Mx Carter anasema kuwa hata hivyo balaa hilo la account yake ya youtube kwa sasa limehamia mpaka kwa msanii mwingine akimtaja shilole  akisema kuwa ndie aliemwambia kuwa Mx Carter ndie alikuwa akichezea account yake hiyo na kusababisha hayo yote.

Sasa kama anagombana na watu kwa style hii hata akija na shida tena siwezi kumsaidia kwa 100% , hapa ninapokwambia kashaanzisha mtiti sehemu nyingine ,amesema kuwa Shilole ndie aliemsababishia yeye aseme hivyo,kwaio sasa hivi hapatani na Shilole kwa mantiki hiyo Shilole hawezi kumpostia video yake tena. -Aliongeza meneja huyo

Akiwa kama mmoja wa wataalamu wa mitandao Mx Carter amesema kuwa kitendo cha mtu kupunguza mashbaiki katika account yako ya youtube ina maana mtu huyo anakuwa ameingia katika server za youtube na ni kitu ambacho akiwezekani.

Hivi karibuni Baraka amekuwa akitapatapa na kutuhumu watu kadhaa akisema kuwa ndio wanaofanya muziki wake ushuke thamani youtube baada ya kuachia ngoma yake mpya ya Sometimes ,huku akituhumu watu hao kuwa ndio wanaochezea account yake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.