Mzazi Mwenza Wa Chege Amwaga Povu Kwa Wanaomtaka Mpenzi Wake

Mzazi mwenzake na msanii mkongwe wa Bongo fleva Chege Chigunda anayejulikana kama Zahra ameshindwa kujizua na kumwaga povu zito kwa mwanamke ambaye amekuwa akimmendea Baba watoto wake.

Zahra alimwaga povu hilo baada ya kuwa na tetesi kuwa kuna mwanamke amekuwa akimtumia meseji za kumtaka kimapenzi Chege.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zahra alimwaga povu hili:

Ifike steji wanawake tubadilike, hivi kwa nini wanawake hatupendani? Kipindi Chege yupo bachela hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kwenda Kwenye social media na kumzungumzia vibaya leo hii amekuwa staa kiasi gani hadi mtake kumuharibia CV yake Jamani? Kipindi hakai na mwanamke mlikuwa mnamuona muhuni sio handsome na maneno kibao ya kashfa kwa kaka wa watu hakuna hata aliokubali kuacha mambo yake nakuamua kumzalia kila mtu alikuwa anamdharau kwa staili yake leo mimi nimeamua kumzalia na kuishi naye mnaanza vitu vya ajabu! Ili baadae muanze kusema wasanii sio ya wanaume mbona kamuacha mzazi mwenzake. Nipumzisheni na DM zenu hakuna aliokamilika hapa duniani unamsema sijui ana wanawake wengi je wewe kwa mtu wako uko peke yako? Ndio kwanza mtoto ana Miezi mitatu mmeanza haya nikizaa wapili simtanirushia mabomu?”.

Chege na Zahra walianika mapenzi yao hadharani Miezi michache iliyopita baada ya kufanikiwa kuzaa mtoto wao wa kike anayeitwa Judah.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.