Mzee Majuto Agoma Kuigiza Tena , Aomba Kuongea Na Waziri na Rais

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini , Mzee Majuto amefunguka na kusem kuwa kwa sasa hana mpango wa kuigiza tena kwa sababu anataka kupumzika na wala hataki kusikia kitu kuhusu sanaa.

Majuto amesema kuwa maamuzi yake hayo kwa sasa ni ya mwisho na hakuna wa kuyabadilisha tena isipokuwa mh mwakyembe au mh raisi magufuli endapo watapata muda wa kuongea nae,lakini si vinginevyo.

download latest music    

Majuto anasema kuw akwa sasa haoni haja ya kuendelea kuigiza lakini kama atapokea ushauri kutoka kwa viongozi hao wawili wakubwa kuhusu sanaa anaweza kuwasilikiza na kubadili mawazo lakini sio mtu mwingine yoyote yule.

Natoa kauli yangu rasmi kuwa sitaku kuigiza tena labda raisi wangu mpendwa Magufuli  au mzee wangu Mwakyembe waniambia hapana endelea ndipo nitawasilikiza,hakuna mtu mwingine wa kunishauri baba yangu alishafariki na mama yangu alishafariki na marafiki zangu wote ni wasanii watupu.

Mara ya kwanza Mzee majuto aliwahi kutangaza kuwa anaachana na kazi ya sanaa na wasanii wengi walimlilia na kumfanya arudishe moyo wake nyuma ili kuendelea na sanaa lakini kwa hapa karibuni Mzee majuto alipatwa na maradhi yaliyomfanya kukaa hospitali kwa muda mrefu hivyo anaona kuwa anahitaji kupumzika kwa sasa.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.