Mzee Majuto Aomba Wasanii na Mashabiki Wamuombee.

Msanii wa maigizo ya  vichekesho na filamu nchini Mzee Majuto amewaomba wasanii na mashabiki zake kuendelea kumuombea kwa sababu hali yake sio nzuri sana pamoja na kwamba ameshatoka hospitali  alipokuwepo kwa ajili ya matibabu yake aliyokuwa  anapatiwa.hata hivyo mzee majuto anasema kuwa alitakiwa kufanyiwa upasuajai lakini ilishindikana kwa sababu ya matatizo aliyokuwa ameyapata daktari wake.

Mzee Majuto aliekuwa akiumwa ugonjwa watezi dume amesema kuwa ugonjwa huo ni hatari kuliko  ambavyo watu wanafikiria kwa sababu unaweza kukutoa Duniani bila hata ya wewe kujua kwaio anaomba watu wamuomee ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

download latest music    

Mzee Majuto alilazwa wiki chache zilizopita katika hospitali ya tumaini jijini dar ambapo mh raisi laikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali  msanii huyo na kmpa pole kitu ambacho pia kilimfariji sana msanii huyo.

Hata hivyo Mzee Majuto ambae kwa sasa yuko nyumbani anasema kuwa february 11 anatakiwa kurudi tena hoispitali kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake na kufanyiwa upasuaji kwa sababu daktari aliyekuwa ana mpatia matibabu alikuwa amefiwa hivyo kufanya kusimammishwa kwa matibabu yake.

Niliruhisiwa jumamosi iliyopita lakini kwakweli bado ninaumwa, tezi dume wala sio mchezo kwakweli.ninachoweza kuwaambiwa na kuwaomba ni kwamba ninaomba mniombee  tu , sala zenu pia zinahitajika.

 

 

,

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.