Mzee Majuto Azungumza Kuhusu Kuzushiwa Kifo

Baada ya kuzushiwa kifo kwa msani wa bongo movies Mzee Majuto, mzee mwenyewe amemzungumza na waandishi wa habari na kukanusha kifo hiko na kusema kuwa yeye bado yuko hai lakini hata kama atakufa anawaomba sana watanzania wamuombee ili aweze kufa kifo  chema.

Akiongea na Global Online tv, mzee majuto anasema kuwa  kuwa anawashukuru watanzania kwa sara zao lakini anawaomba sana waendelee kumuombea huku akiishukuru serikali ya Tanzania kwa matibabu waliompatia.

download latest music    

Ninawaambia watanzania washtute , mimi sijafa mimi mzima jamani,kama mwenyezi mungu atanichukua basi mje mnizike kwa wingi , mniombee ili niende mahali pazuri, mlimpenda sana rafiki yenu kanumba lakini Mungu alimpenda zaidi.

Taarifa hizo ziliazna kusambaa juni 26 mwaka huu lakini mwanae wa kiume aliongea na kukanusha taarifa hizo na kusema kuwa baba yake alikuwa akiendelea vizuri.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.