Mzee Yusuf aeleza watoto wanavyomuulizia marehemu mama yao atarudi lini

Siku kumi zilizopita Mzee Yusuf ambaye alikuwa muimbaji wa nyimbo za Taarabu alimpoteza bibi yake mdogo Chiku Khamis akijifungua mtoto wake wa tatu.

Hata hivyo wanawe ambao ni wadogo bado hawajafahamu kilichotokea kwenye familia yao. Mzee Yusuf amefunguka kusema kuwa sasa hivi watoto hawa wamekuwa wakimuulizia mama yao. Mzee Yusuf aliambia Gazeti la Risasi Mchanganyiko kuwa watoto hao wamekuwa wakimlilia mama yao sana huku wakiuliza alipo.

download latest music    

Aliendelea kusema kuwa alilazimika kuwapeleka kwa ndugu wa mama yao, ili kupunguza machungu yao.

Ninapata taarifa kuwa watoto hawaishi kuuliza alipo mama yao na kila wakikumbuka wanalia, hili ni jaribio kubwa ambalo atalazimika kupigana ili kuhakikisha linaisha salama.

Hata hivyo kwa hivi sasa anataka kuwarudisha nyumbani kwake. Aliendelea kwa kusema,

Nadhani huu muda ambao wamekaa kwa ndugu wa mama zao hao unatosha, hivyo nakwenda kuwachukua ili nikae nao mwenyewe, nianze nao maisha mapya ya bila mama yao kwa sababu nahisi ndiyo faraja yangu kwa sasa. Sijawa na maisha, bado nimechanganyikiwa, hivyo naamini nikienda kuwachukua watakuwa faraja yangu maana nikiwa nao naona niko salama zaidi, watoto wangu nitakaa nao mwenyewe maana mimi ndiye baba yao, watakaa na nani tena kama siyo mimi?

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua