Nafurahi Kuona Wasanii Wa Kike Tukiwa na Ushindani-Nandy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake mpya ya ‘Aibu’ Faustina Charles maarufu kama Nandy amefunguka na kusema anapenda ushindani wa wasanii wa kike.

Nandy ameweka wazi kati ya vitu vinavyo mfurahisha Kwenye muziki huu wa Bongo fleva ni pale ambapo wasanii wa kike wa sasa wanavyoongeza kasi ya ushindani kwenye gemu.

download latest music    

Kutokana na kuwa na ongezeko kubwa la wasanii wa kike tofauti na miaka ya nyuma ambapo sanaa ilikuwa imetawaliwa na wasanii wa kiume na wasanii wa kike walikuwa wa kuhesabika.

Kwenye Interview aliyofanya na Gazeti la Dimba, Nandy amefunguka na kukiri kumekuwapo na ongezeko kubwa la ushindani kati ya wasanii wa kiume na wa kike, hali inayoongeza ladha ya muziki wao.

Nafurahi sana nikiona mwanamke mwenzangu anashindana kipaji na mwanamume, kwangu ni faraja kubwa, kwani tukiendelea hivi tutafika mbali”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.