Nahrel Ataka Wasanii na Vyombo vya habari Kutengeneza Mashabiki.

Msanii kutoka katika kundi la Navy kenzo , Nahrel amefunguka na kusema kuwa siri kubwa ya msanii kupata mashabiki ni kama msanii huyo atawatengeneza ashabiki wake ili kukuza muziki wake na pia kupendwa na mashabiki hao.

Nahrel anasema kuwa inabidi ifike sehemu wasanii wajua vitu gani vinatakiwa kupewa kipaumbele katika muziki na sio kila kitu kama kiki na mambo yasiyovutia mashabiki lakini vile vinavyoweza kuwapa amshabiki hamsa ya kupenda muziki.

download latest music    

Nahrel anasema kuwa wasanii , vyombo vya habari na wadau wa muziki hawaongelei mambo muhimu ya muziki kama matamasha au wasanii kutoa album lakini wamekuwa wakiongelea mambo yasiyo ya msingi ambayo kwa sanii ni kiki tu.

Ukubwa wa tukio katika muziki  utengenezwa na msanii au chombo cha habari na ndio shabiki anaweza kuamini zaidi, na shabiki huamini sana kama chombo cha habari kinaweza kuzungumzia, lakini shabiki hawezi kufatilia kitu ambacho hakizungumzwi.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.