Nai Adai Gigy Money ni Mnafiki na Sio Rafiki Mzuri Kwake

Video vixen maarufu Bongo Nai ambaye pia ni mpenzi wa msanii wa Bongo fleva Moni Centrozone ameibuka na kumtolea povu Gigy Money kwa kudai sio rafiki mzuri.

Gigy Money na Nai walionekana kuwa na ukaribu mkubwa siku za hivi karibuni hasa baada ya Gigy Money kuachana na Mo j na Nai kuachana na Moni centrozone.

download latest music    

Lakini ukaribu huo uliingia mdudu baada ya habari kusambaa kuwa Gigy anatoka na Moni na hata alibadilisha jina lake na kujiita Gigy Centrozone Kwenye Instagram.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, NAi anafunguka na kuweka wazi kuwa ameumizwa na kitendo kilichofanywa na Gigy Money ambaye amekiri kuwa sio rafiki mzuri kwake:

Gigy sio rafiki mzuri kwangu kwa sababu ni mtu ambaye anajaribu kuniongelea vibaya hata kwa Moni ambaye alimposti na kujibadilisha jina na pia kajaribu kumpelekea vitu vya uongo vingi ambavyo vimetufanya mimi na Moni mpaka sasa hatupo sawa.

Na pia naweza kudiriki kusema kuwa Gigy sio rafiki wa kweli kwangu hivyo nimemuweka pembeni nina maisha yangu mwenyewe sihitaji watu wanafiki”.

Nai amekiri kuwa Gigy Money alimtafuta ili wayamalize lakini amesema hataki Tena urafiki naye kwani ameharibu uhusiano wake na mpenzi wake Moni.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.