“Najisikia Vibaya Kushindanishwa na Aslay”- Mbosso

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Hodari’ Mbosso amefunguka na kuweka wazi kuwa anachukia sana kupambanishwa na Aslay.

Mbosso na Aslay walikuwa pamoja katika kundi la Yamoto Band lakini baada ya kundi kuvunjika kila mmoja alienda njia yake lakini mashabiki wamekuwa wakiwapambanisha sana.

download latest music    

Mbosso amefunguka na kusema hakuna kitu kinachomsumbua na kumfanya ajisikie vibaya kama kuona anapambanishwa na Aslay kwa sababu anaona kabisa hawawezi kulingana kwa sababu Aslay ni kaka yake.

Hakuna kitu kinanifanya najisikia vibaya mara kwa mara kama nikaona nashindanishwa na Aslay, Mimi Aslay ni Braza angu, alafu isitoshe mimi nimeanza mziki kama Solo artist nina Miezi Tisa sasa lakini Aslay alianza muziki kama Solo artist tangu mwaka 2011 kwaiyo ni mkubwa sana kwangu mimi bado mchanga mno kwaiyo ukinifanisha naye unakuwa unamvunjia heshima yake na mimi sitaki iwe huvyo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.