Najivunia Miaka Zaidi Ya 20 Kwenye Sanaa Bila Skendo- Maya

Msanii mkongwe wa Bongo movie Mayasa Mrisho maarufu kama Maya amefunguka na kudai hakuna kitu anajivunia kama kufikisha miaka 20 Kwenye sanaa bila hata skendo moja.

Maya ambaye alianza Safari yake ya sanaa katika kikundi cha sanaa cha Kaole, amesema anafurahi sana kwa sababu kama Msanii mkongwe angeweza kushushiwa heshima kama angepata skendo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Maya amefunguka na kudai kwamba nidhamu hiyo ya kuheshimu kazi anayofanya walipata wasanii wa zamani ambao walikuwa wakisimamiwa kwenye vikundi na kuongozwa na wazee kama marehemu mzee Fundi Saidi ‘Kipara’ na Rajab Hatia ‘Pwagu’ ndiyo imemfanya kuepuka mambo ambayo yanaweza kumchafulia jina.

Kiukweli hakuna kitu ambacho ninakiogopa kama skendo, lakini hiyo yote tulifundishwa zamani wakati tukiwa Kaole, ilikuwa ukifanya ujinga tu unaadabishwa na wazee”.

Wasanii wengi wa kileo wameacha skendo zitawale kazi zao kiasi ya kwamba zinafunika viapaji vyao na kusababisha kwa kiasi kikubwa kushuka kwa Kiwango cha sanaa yetu tofauti na miaka ya nyuma.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.