Nandy Adaiwa Kuhongwa Gari La Mamilioni

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT, Faustiana Charles maarufu kama Nandy amefungukia tuhuma alizotupiwa na kudaiwa kuwa gari aliliouza nalo sura hivi karibuni Kwenye mitandao ya kijamii amehongwa.

Wiki iliyopita kuna picha na video zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Nandy akionyesha gari lake jipya alilodai amenunua hivi karibuni aina ya Mercedes Benz E-Class E320 CDI.

download latest music    

Lakini Kumekuwa na tetesi zinazosema kuwa Nandy amenunuliwa gari hilo kama zawadi na kigogo ambaye anamuweka mjini kwa hivi sasa taarifa ambazo Nandy amezikataa kata kata.

Kwenye Interview na Risasi Jumamosi, Nandy alisema kuwa, gari hilo alilinunua kwa zaidi ya shilingi milioni 70 za Kitanzania kwa jasho lake na hiyo ilitokana na kuingia mikataba na makampuni mbalimbali Tanzania yakiwemo ya michezo ya namba, shirika moja kubwa la ndege na mingineyo.

Watu wengi wanajua kuwa kuna mtu ameninunulia hili gari, lakini siyo kweli kabisa, mimi mwenyewe nina madili mengi ya kufanya na ndiyo yameniwezesha kupata fedha za kununua Benz, yaani kifupi ni jasho langu mwenyewe”.

Nandy Amekuwa akifanya vizuri na ngoma yake mpya ya Ninogeshe ambayo imeshika chati mbali mbali nchini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.