Nandy afunguka kueleza msanii anayetamani sana kufanya kazi naye!

Image: Nandy

Nandy ambaye anafanya vizuri kwenye Bongo music kwa hivi sasa anawatisha wasanii wengi. Sio tu kwa urembo wake lakini kwa Sauti yake nzuri ambaye imeipa wimbo wake “one day” uwezo wa kutamba Afrika Mashariki.

Hata hivyo yeye Kama msanii wa kisasa anatamani sana kufanya kazi na wasanii wakubwa. Akizungumza kwenye interview na Clouds FM Top 20 Nandy alimtaja Rayvanny msanii ambaye anatamani kufanya kazi na yeye. Nandy alisema;

download latest music    

 

“Nawaelewa wote lakini kwa haraka haraka nikipewa chance kwa mtu wa WCB kufanya nae ngoma nitafanya na Rayvanny. Nahisi kama tuna chemistry ile ambayo tunaweza tukaendana, yaani ukiwasikiliza mashairi yao wewe ndio unajua unafiti wapi, kwa hiyo mimi naona kwa Rayvanny nafiti.”

Aliendelea kwa kudai kuwa anatamani sana kufanya remix ya wimbo wa Saida Karoli Wa hapo zamani…Iwapo hawezi kupata kufanya kazi na mkongwe wa muziki, Saida Karoli. Nandy alisema,

“natamani sana hata anipe ngoma yake ya zamani niifanyie remix na sijui ni ipi kwa sababu kafumua!, sijui nitaimbaje. Natamani anipe nifanye verse na kama alifanya chorus ibaki pale pale, halafu mimi nirudie zile verse, I hope atakubali.”

Hata hivyo kwa sasa Nandy anatamba na kufanya vizuri na wimbo wake mpya unaojiita ‘Wasikudanganye’.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua