Nandy Ajiingiza Kwenye Ulimwengu wa Ujasiriamali (+picha)

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ameingia rasmi Kwenye ulimwengu wa ujasiriamali baada ya kutangaza bidhaa yake mpya.

Nandy amesema kuwa ameingia ubia na kampuni ya Grace Products inayojihusisha na utengenezaji wa sabuni za kuogea na vipodozi mbali mbali vya asili na yeye atakuwa ni moja ya wamiliki wa kampuni hiyo.

download latest music    

Nandy aliita waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza kuingia ubia na kampuni hiyo ya Grace Products na atakuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo na jina lake na picha zake zitatumika katika baadhi ya bidhaa hivyo kuwataka mashabiki zake wampe sapoti kwa kununua bidhaa hizo.

Ni wiki chache zilizopita Nandy aliongea na kumpongeza Ali Kiba kwa kinywaji chake cha Mo faya Lakini sasa ameamua kufuata nyendo zake.

Hizi ni baadhi ya Picha katika uzinduzi huo:

.

 

.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.