Nandy Alamba Dili Nono na Kampuni Ya Mtandao Wa Simu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na kibao chake cha ‘Ninogeshe’ Faustina Mfinanga maarufu kama Nandy amelamba Dili nono na kampuni ya Halotel.

Nandy amechaguliwa na mtandao wa simu wa Halotel kuwa balozi wao mpya kupiti promotion yao mpya ulioizindua uitwayo, Ninogesha.

download latest music    

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba na msanii huyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni imemchagua Nandy kwa sababu ana uwezo wa kuwa na mchango chanya utakaosaidia kukuza mauzo ya bidhaa na huduma, pamoja na kuimarisha jina la kampuni.

Nandy ni msanii anayekonga nyoyo za mashabiki wake kupitia wimbo wake unaovuma kwa jina la ‘Ninogeshe’ na kumpa umaarufu unamfanya afahamike kwa watu wa rika zote. Unampa umaarufu ambao utasaidia kuiwakilisha vema kampuni ya Halotel“.

Nandy amesema hiyo ni fursa kubwa na ya kipekee kwake kuwa miongoni mwa familia ya kampuni hiyo na kupewa jukumu la kuiwakilisha ipasavyo kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla kutokana na huduma bora za mawasiliano inazotoa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.