Nandy Amkana Dogo Janja na Kumtamani Billinass

Msanii wa kike anaefanya vizuri katika tasnia ya muziki kwa sasa na wimbo wake wa kivuruge, Nandy  amefunguka na kusema kuwa hana mahusiano na msanii Dogo janja kama vile watu ambavyo wamekuwa wakisema katika mitandao ya kijamii.

Kuna baadhi ya watu walikuwa wakisema kuwa kisa cha Nandy kuimba wimbo wa kivuruge ilikuwa ni meseji iliyotumwa kwa msanii Dogo janja baada ya kutemana nae na kwenda kutembea hadi kumuoa Irene uUwoya lakini Nandy amekanusha maneno hayo na kusema kuwa yeye na Dogo janja ni marafiki tu na hawana bifu lolote na wala hana uhusiano nae wowote hivyo hawezi kumuimbia wimbo huo.

download latest music    

Nandy amesema kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Dogo janja na wala hajawahi kumuwazia dogo janja labda wangemwambia kuhusu Billnasss kwa sababu ni msanii anaempenda sana na anatamani sana kuwa nae endapo msanii huyo atamfata na kuelezea hisia zake.

sijawahi kuwa na uhusiano na Dogo janja,ila ni mshikaji wangu tu na sijawahi kumfikiria  labda mngeniambi akuhusu Bilnass kwa sabau ni msanii wa kiume ninaempenda  na ninatamani siku moja awe wangu endapo atanifata lakini.-Alifunguka msanii Nandy.

miezi kadha nyumba nandy na billnass walisemekana kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na kusemekana kuwa walikuwa wakionwa sehemu mbalimbali, hata hivyo kwa upande wa billnass alishawahi kukuri kuwa Nandy ni msanii wa kike pekee ambae anaweza kuwaza kumuoa na anaeona kuwa ana sifa za kuwa mke.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.