Nandy Amwaga Povu Baada ya Habari Kusambaa Kuwa Ameonekana Serengeti na Boss Ruge

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘kivuruge’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya habari kusambaa mtandaoni kuwa ameonekana mbuga za wanyama Serengeti na Ruge.

Siku ya Jana habari zilianza kuenea mtandaoni msanii huyo ameonekana akiwa zero distance na mkurugenzi huyo wa Clouds Fm Ruge Mutahaba ambaye pia ni boss wake pale THT. Baadhi ya watu wanaofanya kazi huko Serengeti walituma ujumbe huu kuthibitisha kumuona Nandy na Boss Ruge:

download latest music    

Mwanamuziki Nandy ni kweli kabisa yupo Serengeti na Ruge nashangaa anavyobisha tena wapo Serengeti Serena waliingua Jumanne. Wapo room namba nane na akibisha tuseme hadi nguo alizovaa na alivyosuka mnafiki Mkubwa tena waliingia hapa mida ya saa nne”.

Baada ya habari hizo kuenea Kama moto wa kifuu Nandy kupitua ukurasa wake wa Instagram alikataa tuhuma hizo na kutoa povu Kali:

Mtu akifanya mziki wake kwa amani bila drama kuna watu wanakuwa hawatosheki kabisa….Hivi mimi ni kichaa mpaka kujiachia kama huyo msambaza habari anavyodai! Kwani suza kitoto. Msu force mambola la watu kusema natoka na boss wangu nalijua leo au ni geni mpaka nijiachie kwenda naye macamp au maclub na kupanda ndege kiufree kama mnavyodai?? Embu tuwe na pliiz kwaiyo mimi nimekuw wa kuja kiasi hicho na mshamba kiasi ya kwamba nikashindwa kufunga hata ushungi basi hata tungepishana kusafiri yeye akatangulia mimi nikafuata nyuma au mnadhani mimi mtoto sana tafadhali tupeane heshima kuna watu hatutaki drama za kitoto na msi force mambo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.