Nandy ataja baadhi ya changamoto anazozipata kwenye muziki

Image: Nandy

Nandy ni msanii ambaye ameanza kutamba Tanzania kwa haraka. Hata hivyo kama wasanii wengine pia yeye a spirit changamoto ambazo ameweza kuzitaja kwenye Interview yake hivi karibuni.

Muimbaji huyu amesema kuwa kwa sasa anajaribu kuwapa mashabiki wake nyimbo ambazo wasanii wengine hawafanyi. Kulingana na yeye inampaswa awe na ubunifu ambao utaweza kumfungulia njia za kupenya Afrika Mashariki.

download latest music    

Aliendelea kwa kusema kuwa changamoto anazopata kwa sasa ni kushindana na wasanii wa kike ambao wamepenya kwenye muziki. Akizungumza naTBC Taifa Nandy alisema,

Nandy
Nandy

“Yaani nikija kutoa wimbo usishuke au uwe juu zaidi, au nifanye ubunifu gani kutofautiana na wenzangu ili niweze kubakia katika nafasi yangu. Wasichana wote kwenye industry wapo katika ushindani  kwa sababu tunafanya biashara moja, kwa hiyo ninapomuangalia mtu kama Maua namuangalia kwa jicho la kama msanii mwenzangu, kwa jicho la kibiashara, kwa hiyo namuangalia kama mshindani wangu.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua