Nandy Atangaza Kuukacha Mziki Ukifika Mwaka 2020

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustine  Charles maarufu kama Nandy amefunguka na kuweka wazi kuwa ukifika mwaka 2020 ataachana kabisa na muziki.

Nandy ambaye aliingia kwenye muziki rasmi kuanzia mwaka 2016 Kupitia Nyumba ya vipaji THT na kutoa ngoma kali ambazo zimemuweka Kwenye ramani kama Msanii bora wa kike Tanzania ametangaza kuachana na muziki hapo baadae.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya gazeti la Risasi Jumamosi, Nandy alisema ndoto yake ni kuwa mfanyabiashara mkubwa Bongo kwani ndiyo yalikuwa malengo yake pindi tu alipoanza kufanya muziki.

Wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo kwamba baada ya miaka mitano niache muziki ili niendeleze biashara zangu, hivyo namshukuru Mungu kwa sababu mpaka sasa nimeshatumia miaka miwili ambayo ni mwaka 2016 na 2017. Kwa hiyo utakapofika mwaka 2020 nitaacha muziki, ila siyo kama nitakuwa sitoi nyimbo hapana nitakuwa natoa lakini kwa mwaka mara moja ili niwe napata muda mzuri wa kusimamia biashara zangu”.

Hivi sasa Nandy anafanya vyema na wimbo wake wa ‘Aibu ambao pamoja na kwamba ni audio tu hauna video umeendelea kumuweka Kwenye ramani kama Msanii bora wa kike Kwenye Bongo fleva.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.