Nandy Awahasa Wazazi Kupenda Kuhimiza Watoto Kuvaa Vitu vya Asili

Mwanadada Nandy ambae amekuwa moja ya wasanii wanaovaa sana nguo za sili na urembo wa sili kama vitenge na mabangili amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake amekuwa aktika mazingira hayo na ndio maana inampa moyo kuendelea kufanya.

Nandy anasema kuwa wazazi wana nafasi kubwa sana ya kuwahimiza watoto wao kupenda vitu vya asili kama watakuwa wakiwakuza katika misingi ya kuvipenda kuliko kuwanunulia vitu tofauti na vile vya asili,

download latest music    

Akitolea mfano wake anasema kuwa tangu akiwa mtoto mama yake amekuwa akivaa mabatiki na vitenge na hata wao wamekuwa wakishonewa nguo hizo na ndio maana amekuwa akiona na kupenda kufanya hivyo.

Mneno hayo ya nandy yanakuja ikiwa ni kuelekea kilele cha tamasha la Urithi Festival linalotegemewa kufanyika mkoani Dodoma mwezi huu.

Mimi napenda sana kuvaa vitu vya asili na ndio maana mmekuwa mkiniona nashona shona,nimekuwa nikiona tangu nikiwa mdogo mamangu amekuwa akitushonea nguo kwaio nimekuwa nakiona na nikakipenda sana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.