Nandy Awatolea Povu Wanaomsema Anabebwa Kimuziki.

Mwanadada Nandy amefnguka na kusema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimtuhumu na kumwambia kuwa amekuwa akibebwa katika muziki na baadhi ya watu na wala sio kipaji chake, Nandy ameonekana kuchukizwa na maneno hayo.

Nandy akiongea na bongo 5 anasema kuwa anashangazwa  sana na  watu wanaongea hivyo  kwa sababu kwa upande wake anajua kabisa kuwa amekuwa akifanya kazi na akitoa ngoma kila mara na nzuri zaidi ni kwamba zimekuwa zikipigwa katika station mbalimbali.

download latest music    

Hayo maneno yao hayanipi tabu yoyote kwa sababu kila siku nasikia kuhusu kubebwa kubebwa lakini nyimbo zangu zimekuwa zikipigwa radioni na zimekuwa zikihit kila kona kwa mfano sasa hivi ninogeshe ina viewers zaidi ya milion 5 kwaio siona kama nabebwa.

Hata hivyo Nandy anasema kuwa haogopi kuongelewa kwa sababu hiyo ni kawaida kwake kama star.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.