Nandy: Bora Nitembee na Bill Nas Kuliko Dogo Janja

Mwanamuziki wa Bongo fleva nchini Nandy anayefanya vizuri kwa hivi sasa na wimbo wake wa ‘Kivuruge’ amefunguka na kudai kuwa yupo radhi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzie Bill Nas kuliko Dogo Janja.

Kutokana na urembo wake na mafanikio yake katika mziki huu wa Bongo fleva mashabiki wengi wamekuwa wakitaka kujua ni nani ambaye ana uhusiano na Nandy kwani amekuwa akificha sana nani ni mpenzi wake.

download latest music    

Kuna habari zilizosambaa sana kwa muda mrefu sasa kuwa Nandy ana uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake ambaye na yeye anafanya vizuri Bill Nas lakini mara kwa mara wamekuwa wote wawili wakikataa tuhuma hizo huku wakisisitiza kuwa nimarafiki wa kawaida tu.

Lakini siku za hivi karibuni pia habari zilisambaa kuwa Nandy ana uhusiano pia na msanii mwingine wa Bongo fleva Dogo Janja ambaye ameimba naye nyimbo siku za nyuma kidogo.

Kwenye mahojiano na LilOmmy Nandy amefunguka na kudai kuwa ni bora awe na Bill Nas kuliko na Dogo Janja;

Hapana wimbo wangu wa Kivuruge sijamuimbia Dogo Janja alafu isitoshe hii nyimvo sijatunga mimi wala sijaiandika kuna mtu aliiandika nikaisikia nikaipenda ndio nikainunua lakini hainihusu mimi alafu isitoshe Dogo Janja ni rafiki yangu yaani hata sijawahi kumfikiria kiivyo yaani bora hata Billnas naweza nikakaa nikamuamgalia nikaona kwa mbali nikaona kama  ninaweza kutembea naye Lakini Dogo janja siwezi kupoteza muda wangu hata kumfikiria”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.