Nandy Na Alikiba Kutwaa Tuzo Za AFRIMA Nigeria.

Usiku wa kuamkia leo Tanzania iliibuka kidedea tena ikiwakilishwa na wasanii wawili Alikiba na Nandy ambao wameweza kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya tuzo za musiki zilizokuwa zikifanyika nchini Nigeria zinazojulikana kama  ALL AFRICA MUSIC AWARDS 2017 (AFRIMA).

Staa wa hit song ya wasikudanganye Nandy ameshinda tuzo moja ya  msanii bora wa kike kwa upande wa Afrika Mashariki huku msanii wa kiume kutoka Tanzania tena Alikiba akiwa ametwaa tuzo mbili yaani katika kipengele cha  Best Artist or Group  in African RnB  and Soul  akiwa na rapper MI na  kolabo bora ya africa  ikiwa ni wimbo wa Aje.

download latest music    

kutoka katika ukurasa wa AFRIMA

Lakini pia nandy ambae alikuwa huko siku chache kabla alionekana kuwa mwenye furaha huku akishukuru kwa mapokezi makubwa aliyoyakuta kitu ambacho hakutegemea kama na yeye anaweza kuwa na fanbase kubwa mpaka nchini tofauti na Tanzania ambapo alitegemewa kuperfom katika jukwaa hilo.

Msanii Nandy akionesha tuzo yake baada ya kuipokea

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.