Nandy na Aslay Wamkosha Mama Samia.

Mwisho wa wiki hii wasanii wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki hasa wimbo wao mpya waliorudia wa Subralkheri , Nandy pamoja na Aslay wamepata bahati ya kukutana na Mh. Mama Samia Suluhu, Makamu wa raisi kwa wimbo huo mzuri ambao umemkosha sana mama huyo.

Aslay na nandy waliamua kuurudia wimbo huo ambao uliimbwa miaka mingi ya nyuma kidogo ,ikiwa  hii ni mara ya pili kwa mara ya kwanza uliimbwa na nasra kidogo mwanamuziki wa taarabu.hata hivyo wimbo huo pia umekuwa ukifanya vizuri katika Radio na Tv station mbalimbali na umekuwa ukiombwa na watu kwa mkupuo.

download latest music    

Mama Samia amesema kuwa amefurahishwa sana na wasanii hao kufanya kazi hiyo kwa pamoja na kuifanya vizuri kabisa na amewaomba waendeelee kufanya nyimbo hizo vizuri na kuacha kujiingiza katika makundi mabaya.

Imekuwa ni kama style kwa sasa kwa wasanii wa bongo fleva kurudia nyimbo za wasanii wa zamani , lengo ni kuwakumbusha mashabiki juu ya wasanii wa wazanii lakini pia kuwaburudisha wazee wa zamani.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.