Nandy- Nategemea Kuolewa Hivi Karibuni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kwa Jina la usanii kama Nandy amefunguka na kuweka wazi kuwa anategemea Kuolewa hivi karibuni.

Nandy amefunguka Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi kuwa kuna mipango kabambe  ambapo ataolewa hivi karibuni huku akigoma kumwanika mchumba’ke akihofia nyakunyaku wa mjini.

download latest music    

Nimewaambia tu ninyi kwa sababu mmeniwahi kuniuliza, ukweli ni kwamba nitafunga ndoa soon, lakini kuhusu mwanaume wangu, naomba nisimwanike kwa sasa”.

Lakini pia Nandy ameongelea furaha yake aliyonayo kwa hivi sasa baada ya Kupitia kipindi kigumu kwenye maisha yake mwezi uliopita.

Unajua nimepita katika wakati mgumu sana, lakini sikumuacha Mungu kabisa na ndiyo maana hata haya yote yanayonitokea ya kupata mikataba na kufanikiwa hadi kununua gari ni kwa sababu kila kitu changu sasa kiko sawa kabisa”.

Mwezi uliopita Nandy aliposti a kipindi kigumu baada ya video yake ya ngono akiwa na mpenzi wake kwa kipindi hiko Billnas kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha kudhalilika kupita kiasi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.