Napenda Sana Mapenzi
Mwanadada Chemical amefunguka na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kuamua kuimba style tofauti na ile aliyozoea kuimba hapo awali ni kwa sababu anapenda sana kusikiliza nyimbo za mapenzi kwa sasa.
Chemical ameyasema hayo alipokuwa akitambulisha wimbo wake wa tila lila ambao kwa kiasi flani jina lake limefanana na lile la Mr blue lakini anasema kuwa haina ufanano wowote hata kama limekuwa na jina sawa kwa sababu hata maneno yake hayafanani kabisa.
Chemical anasema kuwa kbala ya kutoa wimbo huu alimuomba Mr blue kusikiliza kazi hiyo na kutoa ruhusa ya ktumia jina la wimbo wake katika wimbo huo, na hata hivyo anasema kuwa anapenda sana kuimba mapenzi na ndio maana kila anapopata nafasi huimba kwa hisia sana.
Hata hivyo Chemical anasema kuwa sababu kubwa ya yeye kukaa kimya ni kwa sababu alikuwa shule kwa sababu ameamua kurudi shule kwa sasa.