Nataka Kuanzisha Timu ya Mpira :-Gigy Money

 

Msanii wa Bongo fleva nchini, Gift Mwakyusa ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa kupitia watoto wake ana mpango wa kuanzisha timu yake ya mpira kwakuwa, anatarajia kuzaa watoto wengi.

download latest music    

Msanii Gift Mwakyusa maarufu kama ‘Gigy Money’ amesema hayo kwenye KIKAANGONI inayorushwa na EATV kupitia ukurasa wake wa Facebook, ambapo amesema hakumbuki ametoa mimba ngapi kabla ya kufanya maamuzi ya kuzaa na atarajia kuzaa watoto wengi zaidi.

Sikumbuki ni mimba ngapi nimewahi kutoa ila sio ufahari sikuwa na uwezo wa kulea lakini saivi nazaa na nina mpango wa kuanzisha timu ya mpira kupitia watoto wangu”, amesema Gigy.
Gigy ameongeza kuwa alijifikiria kutoa ujauzito wa mtoto wake wa sasa lakini hakufanikiwa kufanya hivyo, na kuanzia sasa ameamua kuzaa kwakuwa anaweza kulea

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.