Nataka Mume Sipendi dhambi-Khadija Kopa

Mwanamama Khadija kopa amefunguka na kusema kuwa kwa sasa anaona bora atafute mume wa kumuoa na kwamba anataka mwanaume awe kuanzia miaka 40 kwenda juu kwa sababu hataki vijana maana hana muda wa kufundisha tuition.

Sijaolewa ila sitaki kusomesha tuition, nataka mwanaume awe kuanzia miaka 40 kwenda juu, mwenye mapenzi ya dhati na huba, mwenye kujali na kujua nataka nini.atakae weza kujali familia yangu na watoto wangu , awe mnene kidogo  sio mwembamba awe na rangi yoyote na awe wa kabila lolote mimi sio mbaguzi hata kidogo.

Khadija Kopa pia amesema kuwa anataka mwanaume ambae ni mfanya kazi maana hataki mwanaume wa kukaa nyumbani tuanamsubiri yeye ndo amltee chakula na kila kitu.maana maisha ya sasa ni magumu sio ya kutegemea upande mmoja tu.

download latest music    

Hata hivyo akitoa sababu ya kutokuolewa mpaka sasa tangu mume wake amefariki ni kwa sababu anaogopa na ana wasiwasi sana na wanaume wa sasa.

Nina wasiwasi sana na wanaume wa sasa kwa sababu huwa nawaza je atakuwa na huba kama mwanaume wangu wa kwanza ambae sasa hivi ni marehemu.na ndio maana nimekuwa nikifiria sana kwa sababu mume wangu alikuwa na huba sana, na mwenye kunijali sana , nimekaa nae miaka yote  hatujawahi kugombana nae.Nilikuwa natamani sana kumuona akinuna lakini ananuna vipi?

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.