Natamani Kupata Mtoto Lakini Sina Mpango Kwa Sasa.-Lulu Diva

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Lulu Diva amefunguka na kuzungumzia tetezi zinazoendelea kusamba juu yake kuhusu swala la kutelekeza mtoto wake kijijini na kwamba kutokana na umbali wake  na mtoto imefikia hatua mtoto huyo amekuwa akimwita dada badala ya mama.

Lulu anasema kuwa watu hawajui kuwa hata yeye anatamani mtoto kwa sababu ni baraka kutoka kwa mungu  na   kwamaisha ya sasa hivi kuwa na mtoto ni kuwa na dili kubwa sana kwa sababu anaweza kuwa ambasador wa kampuni flani hivyo ikakusaidia katika malezi pia.

download latest music    

Nimeona hizo taarifa sana katika mitandao lakini sio kweli kuwa mimi nimetelekeza mtoto,kwangu pia ni suprise kwa sababu kutoka kwa mwenyezi mungu mtoto ni zawadi na kwa maisha ya sasa hivi kutupa au kukana mtoto ni ushamba kwa sababu anaweza kuwa balozi wa mabenki , au kampuni flani.

Hata hivyo Lulu Diva anasea kuwa amekuwa akitamani kupata mtoto lakini hana izo plani kwa sasa kwa sababu muda wa kuzaa kwake bado.

Mimi mwenyewe natamani mtoto lakini sina mpango kwa sasa hivi  naona muda bado ila sina mtoto anaeniita dada.nina watoto wa mama zangu wadogo ambae nilimlea na sasa hivi yuko zanzibar, pia kuna mtoto wa dada yangu na wengine wengi ambao wamekuwa wakija kwangu na mimi nina kaa nao na kutoka nao.

Lulu anasema kuwa watu wamekuwa wakisema kuwa  anamficha mtoto mara hamjali mtoto wake lakini hiyo sio kweli lakini anategemea kupata mtoto baada ya miaka mitano.

Kwa sasa sina plani za kupata mtoto kwa sababu niko kwenye plani za kutafuta baba,labda baada ya miaka mitano.na hata mwennzangu nikimuuliza namuona hana muda kwa sasa.

Lulu Diva alipoulizwa kwanini anasubiri muda mrefu hivyo mpaka muda wa kupata mtoto na yeye alijibu.

Tunahitaji kuwawekea na kuwatengeneza mazingira mazuri watoto wetu,sio tunazaa tu kwa sababu tuna uwezo wa kuzaa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.