Natamani Kushinda Tuzo Ya Heshima- Aslay

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana hivi sasa Aslay amefunguka kuwa anatamani sana kama atafanikiwa kupata tuzo basi apate tuzo ya heshima.

Aslay amekuwa akifanya vizuri kimuziki tangu atoke kwenye kundi la Yamoto Band, kila nyimbo ambayo amekuwa akitoa zimekuwa zikifanya vizuri kiasi ya kwamba amewekwa kwenye ramani ya wasanii bora wa Bongo fleva wanaofanya vizuri.

download latest music    

Pamoja na mafanikio hayo Aslay hajawahi kushinda tuzo yoyote hii inaweza Ikawa sababu ya ufinyu wa tuzo nchini ambazo zinatambua mchango wa wasanii mbalimbali na wadau.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv Aslay amefunguka haya kuhusu juu yake ya kuchukua tuzo Tanzania:

Nafikiri kuna tuzo nyingi sana zinatokaga Tanzania na mimi sijawahi kuchukua tuzo yoyote kubwa Tanzania lakini naamini siku nitakayopata tuzo ya heshima ndio nitajiona mimi nimekuwa msanii mkubwa na nitaweza kujishindanisha na wasanii wengine wakubwa”.

Lakini pia Aslay amefunguka kuhusu mipango yake ya kutoa Albamu ambapo ameweka wazi kuwa tayari nyimbo zake za kukaa kwenye Albamu zimeshatimia hivyo yupo kwenye michakato.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.