Natamani Kuzaa na Mtoto Kwanza wa Zari – Gigy Money

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amemtolea povu zito Mzazi mwenza wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady.

Gigy alianza kumtolea povu Zari wiki iliyopita Kwenye mitandao ya kijamii baada ya Zari kudai hataki kuwekwa kundi moja na Gigy.

download latest music    

Lakini inaonekana kama bifu la Gigy kwa Zari halijaisha kwani ameendelea kumuongelea mbovu Kwenye mitandao ya kijamii ambapo sasa ameibuka na kudai anataka kuzaa na mtoto wa kwanza wa Zari ili awe bibi wa mtoto wake.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Gigy amemwagia povu hili Zari:

Zari mimi nakuahaidi kitu kimoja lazima ni we na mtoto wako wa kwanza ili uwe bibi wa mtoto wangu halafu ndio utaniheshimu na ndio maana sitaki kuongea sana maana atakuwa mama mkwe wangu na hatoamini kwa njia yoyote ile mwanangu atakuwa mrithi wa hizo hela anazoringia na kama siwezi kuwa Bosslady kwa njia moja basi nitakuwa hata kwa urithi”.

Zari ni mama wa watoto watano ambao watoto wake watatu wa kiume alizaa na Marehemu Ivan na watoto wake wawili wadogo amezaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.