Nay Ana Wanawake Wengi Sana.:Nini.

Mwanadada nini mbae hivi karibuni alijikuta akiingia matatani baada ya kuamua kutangaza katika mitandao na vyombo vya habari kuhusu kuwa single na kwamba ameachana na nay wa mitego ambae alikuwa mpenzi wake na mahusiano yao waliyafanya kwa siri kwa muda wote.

Huku watu wakihoji kwa nini ilikuwa siri na sasa hivi wameachana na wameamua kutangaza au kwanini wawili hao wameachana, ndipo Nini alipoamua kufunguka kwa waandishi na kusema kuwa swala kubwa ni kutokana na tabia ya Nay wa mitego kutokuwa na mapezni ya kweli kwake na kwamba amekuwa na mahusiano na wanawake wengine wengi.

download latest music    

Nay ana wanawake wengi sana , nimevumilia na nikaona kuwa basi kila mtu na achukue hamsini zake tu,nimeshamsisitza zaidi ya mara mbili lakini nikaona hanisikilizi kwaio nimeona bora nikae pembeni’ Aliongea Nini alipokuwa akihojiwa na Sam misago.

Pamoja na kwamba Nini aliwahi kugombana na uongozi wake kwa sababu ya uhusiano wake na Nay na kuwafanya wawili hao kuanza kufanya kazi pamoja, Nini anasema kuwa swala hilo halimaanishi kuwa  limekwamisha na kuua muziki wake bali yuko pale pale.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.