Nay wa Mitego Akanusha Kufungiwa , Asema Anatakiwa Kufanya Marekebisho

Baada ya uwa akiitwa BASATA kila siku na hata kupewa barua na baadae kutosema kitu chochote hadharani, msanii Nay wa mitego amefunguka na kuelezea kuhusus sababu za kuwa anaitwa BASATA mara kwa mara tangu wimbo wake mpya ulipotoka hivi karibuni.

Nay wa mitego anasema kuwa wimbo wake mpya haujafungiwa lakini kuna baadhi ya sehemu inabidi kurekebisha na kuutoa tena ukiwa hakuna baadhi ya vipande.

download latest music    

Nay wa mitego anasema kuwa “kikao kilikuwa ni kwa ajili ya wimbo wa alisema mabao haujafungiwa lakini siwezi kuongea mambo mengi sana kwa sababu kuna viongozi tulikuwa nao kwaio hao wataweza kuongea kile tulikuwa tunakiongea huko.”

Hata hivyo Nay wa mitego anasema kuwa kuteuliwa kwa baadhi ya wasanii kuwakilisha wasaii katika uongozi wa BASATA ni jambo zuri lakini hawezi kuliongelea kwaio bora wakae kimya waangalie jinsi wasanii hao pia watakavyoweza kufanya kazi.

Mara ya kwanza Nay wa mitego alipoitwa na BASATA aliwahi kuposti picha ambayo kidogo ilileta wasiwasi kwa mashabiki wakidhani kuwa wimbo wake mpya umefungiwa katika vituo vya habari.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.