Nay wa Mitego Kajibu Povu la Godzillah

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego, amejibu rasmi povu lililotolewa na msanii mwenzake wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana Godzillah.

Nay wa Mitego ameachia rasmi ngoma yake jumatatu hii inayoitwa Mikono Juu cha ajabu kilochotokea hapo ni kwamba Nay alipoweka wimbo ule kwenye ukurasa wake wa Instagram Godzillah aliibuka na kudai wimbo ule mbaya lakini hata alipohojiwa na kituo kimoja cha redio alisema Tena kuwa wimbo huo ni mbaya.

download latest music    

Baada ya povu hilo kila mmoja alitegemea Nay wa Mitego atapanick na kumtolea povu zito lakini imekuwa tofauti sana kwani alipohojiwa alisema haoni shida kwani kila mtu ana mtazamo wake binafsi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Nay alifunguka yafuatayo:

Kwanza kwa nini nipanick kisa kaniambia ngoma mbaya? Huo mtazamo mtu anatoa ule anaoona yeye huwezi kupanick utakuwa sio mtu unayefanya kitu kwa ajili ya watu na ukipeleka kitu kwa watu wengi sio kila mtu atapenda alafu mimi nafanya kitu kwa ajili ya watu wengi and then mimi nawajua watu wangu ninaowaimbia lakini pia naamini kizuri hakipendwi na kila mtu asikwambie mtu Yesu mwenyewe alipingwa itakuwa mimi NAy wa Mitego?”.

Lakini pia ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Godzilla na kuna nyimbo zake nyingi anasikiliza pia amesisitiza hana muda wa kukaa na kutengeneza bifu na mtu yeye yupo kikazi kwaiyo anachukulia comment ya Godzilla kama ya shabiki yoyote.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.