Ndoa Ya Chalz Baba Yadaiwa Kuingia Mdudu

Msanii wa muziki wa Bendi Charles Gabriel maarufu kama Chalz Baba aliyejizolea umaarufu Kwenye bendi ya Mashujaa amedaiwa kuwa Kwenye utata kuhusu ndoa yake.

Global Publishers wanaripoti kuwa Chalz Baba na mke wake Rehema Sospeter wamemwagana kisa ni maugomvi ya kila siku ambayo hyaishi ndani ya nyumba.

download latest music    

Lakini pia inadaiwa baada ya wanandoa hao kuachana Chalz Baba Kurudisha mapenzi kwa mzazi mwenzake ambaye pia ni msanii wa Bongo movie Husna Sajent.

Unajua Chaz na mkewe huyo mara nyingi wamekuwa wakigombana mara kwa mara kisha wanawekwa sawa wanarudiana tena. Lakini safari hii inaonekana wazi kuwa ndoa yao haipo tena, kwani mwanamke huyo kabeba kila kitu ndani kaondoka na ni muda mrefu sasa hawaishi pamoja na mwanamuziki huyo amerudisha mapenzi kwa Sajenti”.

Baada ya tetesi hizo kusambaa gazeti hilo lilimsaka Husna Sajent ili kujua kama jambo hilo Kiba ukweli ambapo alikataa tetesi hizo na alipoulizwa zaidi alikata simu.

Lakini pia Chalz Baba aliweka wazi kuwa yeye mke wake wamegombana Lakini anaamini watayaweka mambo sawa na Kurudisha mapenzi yao kama mke na mume.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.