Ndoa Ya Dogo Janja Na Uwoya Ni Kiki

Ikiwa bado kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusu ndoa ya msanii wa muziki Dogo Janja na mwana bongo movie Irene Uwoya, ebu tuangalie jinsi wasanii hawa ambavyo wanataka kuchanganya akili za mashabiki na watu wanaowapenda lakini wanashindwa kufunguka na kusema ukweli wa mambo yao yote.

Baadhi ya vyombo vya habari vilianza kuwatafuta wasanii hawa mara tu baada ya picha za msanii Irene Uwoya kusambaa zikionyesha amevaa gaunu la harusi.alipopatikana dodgo janja alijibu tu kwa mkato na kusema yeye hajui chochote.Jitihada zilipoendelea irene uwoya alipatikana na moja ya waandishi wa gazeti pendwa nchini, katika simu irene alijibu” mimi ni wa kuolewa, na ntaolewa na nani?” hata hivyo mwanadada huyo aliongezea na kusema kuwa hiyo ilikuwa ni movie tu inachezwa.

download latest music    

Madee akiwa kama mtu wa karibu kabisa na Dogo Janja alikuwa ni moja ya watu waliokwepa kwa muda mrefu kutoa taarifa zozote kuhusu ndoa ya Dogo Janja lakini baadae katika ukurasa wake wa instagram Madee aliposti picha yenye kuashiria kujua kiundani tukio ilo

Ndoa ni jambo la kheri, itakuwa ni tatizo kama inakuwa vigumu kwa msanii huyo kuweka wazi swala lake la ndoa hasa mwanaume wake anaeenda kukaa nae katika ndoa hiyo.Leo tarehe 30 Oktoba, Irene Uwoya aliposti picha yake nyingine na kusema kuwa ameolewa na mwanaume anaempenda huku akimshukuru na kumtag dogo janja kuwa ndie mwanaume wa ndoto zake.

Kwa kumbukumbu zinazoonyesha,katika akaunti ya instagram ya mwandada Irene Uwoya zipo baadhi ya picha zinazohusiana na ndoa iyo, moja ya picha hizo zilionyesha kadi za harusi hiyo, je ni kweli tunashindwa kuhoji mbona jina lililopo katika kadi ni tofauti na jina la mtu tunaeambiwa kuwa ndie aliefunga nae ndoa.Nani amegundua hili

Hii ni kadi ya harusi  ya Irene Uwoya , ambae inavyoonyesha na kwa jinsi ilivyosemekana ni kuwa alibadil jina na kuitwa Sheila baada ya kuabdili dini na kuamia upande wa mwanaume anaemuoa.

Nadhani kuna kitu hapa wasanii hawa wanataka kutuchezea,kuwa wazi ni vizuri zaidi ingawa italeta gumzo sana kutokana na umri wa Dogo Janja na irene uwoya ,lakini pia wawili hawa walishasikika mara nyingi wakikanusha tetesi za kuwa wapenzi.je nini kinaendelea?, kwanini Irene hataki kumuweka wazi mwana harusi?, au wanatengeneza kiki kutokana na mitandao inavyowapa muda mwingi kuwazungumzia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.