Ndoa Ya Thea na Mike Yafika Pabaya

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea amekiri ndoa yake na Muigizaji mwenzake Michael Sangu kufika  sehemu mbaya na kutaka ivunjike kanisani.

Thea amefunguka kuhusu ugumu aliopitia katika ndoa yake na jinsi alivyoichoka mpaka kufikia hatua ya kutaka Kubeba mimba ya mwanaume mwingine ili mradi tu Ndoa hiyo iweze kuvunjika.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Thea alisema utaratibu wa ndoa za Kikristo hautambui talaka ndiyo maana tangu amemwagana na mumewe hajaolewa kwa sababu ya kifungo hicho cha sheria za dini ambapo sasa ameamua ‘kujilipua’ ili apate mume mwingine.

Unajua kanisani kama mmetengana na mume halafu ukaenda kuzaa na mwanaume mwingine ndoa inakuwa imeshavunjika tayari, sasa hivi nina mpenzi na ninataka nibebe mimba yake; hapo ndiyo ndoa na Mike itakuwa imefikia ukingoni”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.