Ndoa Ya Zamaradi Yadaiwa Kuzua Ugomvi Kwenye Familia

Ndoa ya mtangazaji wa Clouds FM na mdau wa filamu za kibongo, Zamaradi Mketema imedaiwa kuzua ugomvi mzito kwenye familia yake.

Wiki chache zilizopita Zamaradi aliwashtua wengi mara baada ya kuolewa ghafla bila taarifa na pia iliwashtua wengi kwa sababu ilikuwa inajulikana kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba wa watoto wake wawili ambaye ni mkurugenzi wa Cloufs Fm, Ruge Mutahaba.

download latest music    

Habari zilizoenea hivi sasa zinadai kuwa ndoa hiyo imeleta ugomvi kwenye familia ya Zamaradi hadi kupelekea baadhi ya ndugu zake kumsusa. Ndugu wa karibu wa Zamaradi waliomba majina yao yahifadhiwe wameiambia Za moto moto news kuwa ndugu upande wa baba yake hawako naye vizuri kwani wanadai hawakushirikishwa wala kualikwa kwenye ndoa yake kitendo ambacho kilichowauzi.

Inadaiwa kuwa ugomvi kwenye familia ulianza pale ambapo Zamaradi aliamua kuolewa na mume wake wa sasa ilhali walikuwa wameshapokea mahali ya Ruge. Zamaradi alipopigiwa ili kuhakikisha habari hiyo alijibu kuwa;

Hakuna kitu kama hicho, kwani waliokuwa ndugu zangu wote niliwaalika na walihudhuria kwenye ndoa yangu kama kawaida”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.