Ney Wa Mitego Afunguka Kuuza Magari Yake Yote

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Ney wa Mitego hivi karibuni amekuwa akionekana kuwa akitembea kwa miguu na kukatiza katika mitaa mbalimabli huku kukiwa na tetesi kuwa ameuza magari yake yote aliyokuwa akitumia kwa usafiri.Hata hivyo wapo baadhi ya mashabiki walioanza kusema kuwa inawezekana msanii huyo amefulia hivyo ameona njia sahihi kwa sasa kurudi kiuchumi ni kwa kuuza magari yake yote ili kuweza kujimudu katika swla la kipato.Baada ya kuzuka kwa maneno hayo  msanii huyo ameamua kufunguka na kuongelea swala hilo kiundani huku akikubali ni kweli kuwa ameuza magari yake yote lakini hakuweza kuweka wazi sababu zilizomfanya auze magari yake yote.

Akiongea na channel ya EATV, msanii Ney wa Mitego amesema kuwa”kila mtu anazungumza lake ujue,lakini kama kuuza nimeuza kwa sababu zangu binafsi za kimsingi.Nimeamua kuachana na magari na nimeamua kupanda daladala na bajaji na hayo ndo maisha yaNgu ambayo nilikulia, unajua mimi nimezaliwa katika maisha ya kawaida sana, na mtaaa ndo umenilea” alizungumza Ney wa Mitego.

download latest music    

Hata hivyo akiongezea kwa undani zaidi Ney wa Mitego anasema kuwa endapo atakuwa akionekana mitaani basi watu wasisiste kumpa lifti maana ndio maisha ya kusaiidiana,”watu waasichoke kunipa lifti wakiniona barabarani, au wasishangae wakiniona natembea kwa miguu” aliongezea Ney wa Mitego.

Hivyo basi kwa baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakihofia labda msanii wao amefulia, basi waridhike na majibu ya msanii huyo kuwa kwa sasa ameamua arudi katika maisha yake ya kawaida ya mtaani na nadhani hii itakuwa njia sahihi zaidi kwa msanii huyu kuwa karibu na mashabiki wake kuliko ambavyo angekuwa akitumia gari lake.

Ney wa Mitego ni mmoja wa wasanii wanafanya vizuri katika nyimbo zake ambapo hivi karibuni ametoa vibao kama ‘Maku-zi’ ambao umekuwa ukifanya vizuri katika vituo mbalimbali vya Radio na Televisheni, lakini Ney wa Mitego  ni mmoja wa wasanii anaesifika kwa kusema ukweli juu ya kitu chochote kinachomkwaza bila kuogopa kitamlenga mtu gani.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.