“Ni gonjwa ambalo mimi bado napambana nalo” Chid Benzi afunguka kuhusu vita yake dhidi ya utumiaji wa dawa za kulevya

Utumiaji wa dawa za kulevya ulifanya afya ya Chid Benzi kuzorata kwa kiasi kwamba alikonda sana, picha zake akiwa ameathirika na dawa hizo ziliwashtua watu wengi zilipotea katika mitendao ya kijamii.

Chid Benzi akiwa ameathirika na utumiaji wa dawa za kulevya

Chid Benzi bado anapambana na madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya. Rapa huyo amefunguka kuhusu vita yake dhidi ya utumiaji wa dawa hizi.

download latest music    

“Unajua kwanza hili janga ambalo mimi niko nalo ni ugonjwa na ni ugonjwa ambao ni mgumu sana, halafu vilevile unaendana na kichwa cha mtu na maisha halisi ya mtu jinsi anavyoishi, kwa hiyo ugonjwa wenyewe unaendana na vitu ambavyo unafanya kila siku mpaka unajikuta unaingia tena kwenye mambo hayo. Kwangu mimi kuna vitu vingi ambavyo vilichanganyikana hapo katikati vilivyopelekea mimi kuchanganyikiwa na kurudi kule, lakini bado ni gonjwa ambalo mimi napambana nalo kuliondoa napigana nalo kwa hiyo watu wajue Chid anapigana nalo hili jambo” alisema Chid Benzi.

Chid Benzi akiwa sawa

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere