Ni kweli Hamisa Mobetto anaujauzito wa Diamond Platnumz?

Hamisa Mobetto amejipata tena akisingiziwa kuwa yeye na baba Tiffah wanatoka kimapenzi. Kuzidisha mara hii mrembo huyu anasemekana kuwa anamtarajia mtoto na mkali huyo wa Wasafi records.

Hamisa, Diamond na Zari
Hamisa, Diamond na Zari

Kulingana na fununu mitandaoni hii ndio shida ambayo imemfanya Diamond Platnumz na Zari Hassan kutosikilizana. Hapo awali ilisemekana kuwa wapenzi hao walikosana baada ya Diamond Platnumz kutohudhuria mazishi ya Ivan Don lakini inaonekana kuwa kuna taarifa ambazo mashabiki hawajui kwa sasa.

download latest music    

Hata hivyo hakuna anayejua ikiwa Hamisa Mobetto anamtarajia mtoto wake wa pili na kama ni kweli, hatujui ikiwa mtoto huyu ni wa Diamond Platnumz.

Mamake Diamond Platnumz pia anasemekana kuwa ameridhia mwanae kuwa na Hamisa Mobetto na iwapo hii ni kweli basi Nillan akokaribu kupata mdogo wake!

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua