“Nikifa Nizikwe na Ray na Awasomeshe Watoto Wangu”- Steve Nyerere

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mwanaharakati wa siasa Steve Nyerere ameibuka na kudai hawezi kuacha kusimamia misiba ya watu na msiba wake anataka msanii mwenzake ausimamie.

Steve ameibuka na hili baada ya sakata lake lililompata siku chache za nyuma baada ya kugubikwa na skendo ya kuiba pesa za Michango ya rambirambi.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Steve amesema kitendo hicho cha kusimamia misiba kimeweza kwa namna moja au nyingine kumfanya pia awe karibu na watu wazito nchini ambao wanamuunga mkono kwenye kujitolea kwake.

Sitaacha kusimamia misiba ng’o, wanaosema waache waseme watachoka. Ninasimamia misiba kwa sababu ninafahamu na mimi ipo siku nitaondoka na watu watasimamia msiba wangu. Niseme tu wazi hata kama nikiondoka leo nataka Vincent Kigosi ‘Ray’ asimamie na kuwasomesha wanangu“.

Steve Nyerere amekana kabisa skendo za yeye kudhulumu pesa za rambirambi na kudai akikusanya basi hufikisha kwa wahusika.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.